KITAIFA
DUNIA KUSHUHUDIA HOTUBA NZITO YA LOWASSA LEO
FRIDAY, OCTOBER 23 2015, 0 :
MGOMBEA urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa, leo atalihutubia Taifa kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, redio na mitandao ya kijamii.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene, alisema kupitia hotuba hiyo, Lowassa atazungumzia Tanzania mpya ambayo itatokana na mabadiliko makubwa ya kimfumo, kiutawala na utendaji wa Serikali atakayoiunda baada ya Watanzania kumpatia dhamana ya kuwa Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu na Kiongozi Mkuu wa Serikali Oktoba 25, mwaka huu.
"Huu ni Uchaguzi Mkuu wa mabadiliko ya kuhitimisha utawala wa nusu karne wa CCM ili kuliandaa Taifa na uongozi mpya ambao utatoa wa kuliondoa Taifa katika umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi ambao unawatafuna Watanzania.